Swali: Maovu mengi yanayopatikana ndani ya nchi ya Tawhiyd chanzo chake ni serikali na watawala wake sio viongozi wa Salafiyyuun.

Jibu: Majibu yetu dhidi yao ni kama wale waliomwambia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba ni mwendawazimu na mshairi. Ni kama alivosema mshairi:

Mawingi hayadhuriki na

kubweka kwa mbwa

Leo hakuna nchi kama nchi yetu inapokuja katika kutekeleza Tawhiyd na kuhukumu kwa Shari´ah. Hata hivyo haikusalimika na maovu kama ilivyo ulimwenguni kote. Bali mpaka Madiynah wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walikuweko baadhi ya watu ambao ni waovu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hujj al-Qawiyyah ´alaa Wujuub-id-Difaa´ ´an-id-Dawlah as-Su´uudiyyah, uk. 108
  • Imechapishwa: 01/04/2024