Fir´awn na mke wake kafiri

Swali: Mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) amesema kuwa mwanamke ambaye ameolewa na kafiri basi wanatakiwa kutenganishwa. Fir´awn alikuwa kafiri na mke wake alikuwa muumini na Allaah hakuwatenganisha…

Jibu: Haya hayakutokea katika Shari´ah ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hii ni Shari´ah ya zamani. Shari´ah yetu inatofautiana na Shari´ah za watangu wetu. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا جَاءَكُمُ الْمُؤْمِنَاتُ مُهَاجِرَاتٍ فَامْتَحِنُوهُنَّ ۖ اللَّـهُ أَعْلَمُ بِإِيمَانِهِنَّ ۖ فَإِنْ عَلِمْتُمُوهُنَّ مُؤْمِنَاتٍ فَلَا تَرْجِعُوهُنَّ إِلَى الْكُفَّارِ ۖ لَا هُنَّ حِلٌّ لَّهُمْ وَلَا هُمْ يَحِلُّونَ لَهُنَّ

”Enyi mlioamini! Wanapokujieni waumini wa kike waliohajiri, basi wajaribuni. Allaah anajua zaidi imani zao. Mkiwatambua kuwa ni waumini wa kike, basi msiwarejeshe [Makkah] kwa makafiri – wao si [wake] halali kwao [hao makafiri] na wala wao si [waume] halali kwao.”[1]

Hii ndio Shari´ah yetu.

[1] 60:10

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (37)
  • Imechapishwa: 27/07/2023