Mume amekufa kabla ya kukaa chemba na mke

Swali: Mwanaume amemuoa mwanamke kisha akafa kabla ya kumwingilia. Je, ni mwanamke huyo analazimika kukaa eda?

Jibu: Ndio. Akimuoa mwanamke kisha akafa kabla ya kumwingilia, anazingatiwa ni mke wake; atamrithi na atakaa eda ya kufiwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (37)
  • Imechapishwa: 27/07/2023