Fatwa ya wasiokuwa na elimu kuhusu eda ya mjane

Swali: Je, ni kweli kwamba mwanamke aliye ndani ya eda hatakiwi kupanda ju ya paa, hatakiwi kutazama mwezi wala hatakiwi kabisa kuwazungumzisha wanamme wa kando naye?

Jibu: Hii ni fatwa ya watu wajinga. Hapana. Yote haya si sahihi. Inafaa kwake kupanda juu ya paa, kukaa bustani na mfano wa hayo. Hakatazwi isipokuwa yale aliyokatazwa na Shari´ah, na si yale aliyokatazwa na wasiokuwa na elimu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (40)
  • Imechapishwa: 05/05/2023