Swali: Ni fatwa ipi inachukuliwa ikiwa waulizaji wawili wametofautiana katika fatwa nyingi?

Jibu: Ile iliyoafikiana na haki na ambayo imeafikiana, dalili za Kishari´ah na Qur-aan na Sunnah:

فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ

”Mkizozana juu ya jambo, basi lirudisheni kwa Allaah na Mtume.”[1]

وَمَا اخْتَلَفْتُمْ فِيهِ مِن شَيْءٍ فَحُكْمُهُ إِلَى اللَّـهِ

”Jambo lolote lile mlilokhitilafiana kwalo, basi hukumu yake ni kwa Allaah.”[2]

Ikiwa ana shaka, basi anauliza anayemdhania kuwa yuko karibu, mjuzi na mwenye utambuzi zaidi. Ajitahidi na achunguze.

[1] 04:59

[2] 42:10

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25139/بماذا-يعمل-عند-اختلاف-فتوى-المفتين
  • Imechapishwa: 06/02/2025