Hali mbili ambazo Sujuud ya kusahau inakuwa baada ya Tasliym

Swali: Ni lini Sujuud ya kusahau inakuwa kabla na baada ya salamu?

Jibu: Sujuud inakuwa kabla ya salamu isipokuwa tu katika hali mbili, jambo ambalo ndio bora zaidi:

1 – Akitoa salamu kwa kupunguza Rak´ah moja au zaidi, basi akamilishe na asujudu sijda ya kusahau baada ya salamu.

2 – Akijengea dhana yake kubwa. Katika hali hiyo atakamilisha swalah, kutoa salamu kisha atasujudu sijda ya kusahau.

Hali nyengine zote inakuwa kabla ya salamu. Ndio bora zaidi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25135/متى-يكون-سجود-السهو-قبل-السلام-ومتى-يكون-بعده
  • Imechapishwa: 06/02/2025