Maana sahihi ya kuimba kwa Qur-aan

Swali: Kuna mtu anaimba Qur-aan kama mtindo wa muziki. Je, anakufuru kwa kitendo hicho?

Jibu: Hili halijuzu. Lakini huenda amefahamu makosa:

“Si katika sisi yule ambaye haimbi kwa Qur-aan.”

Maana yake ni kuboresha sauti. Haina maana kwamba anaiimba kwa tungo za mashairi na nyimbo, hapana. Ni kosa. Azinduliwe ya kwamba ni kosa. Hakufuru kwa kitendo hicho. Lakini afundishwe ya kwamba jambo hilo ni kinyume na Sunnah na ni kosa na kwamba kuimba kwa Qur-aan kunamaanisha kuifanya sauti na kisomo kuwa kizuri.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25140/ما-حكم-من-يغني-بالقران-على-لحن-الموسيقا
  • Imechapishwa: 06/02/2025