Fadhilah za njaa na mafungamano yake na kuipa nyongo dunia

Swali: Mtunzi wa kitabu ameweka kichwa cha khabari kinachosema ”fadhilah za kuwa na njaa”. Je, kuwa na njaa kuna ubora kwa dhati yake?

Jibu: Ndio, ni kujinyima (الزهد) kwa ajili ya mambo ya ziada ambayo yanamshughulisha mtu kutokamana na Aakhirah. Kujinyima katika mambo ya haramu na yanayochukiza na kujinyima juu ya mambo yanayomzuilia mtu kutokamana na Aakhirah. Kama alivosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Ipe nyongo dunia atakupenda Allaah na vipe nyongo vile vilivyoko kwa watu watakupenda watu.”

Swali: Kuna Hadiyth ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anamuomba Allaah amuhifadhi kutokamana na njaa akasema:

”Ee Allaah! Mimi najilinda Kwako kutokana na njaa.”

Jibu: Hayapingani. Kuipa nyongo dunia hakupelekei kuwa njaa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22211/هل-للجوع-فضل-وما-صلته-بالزهد
  • Imechapishwa: 12/11/2022