Fadhilah za kumfuturisha mfungaji Ramadhaan

Swali: Je, mfungaji ambaye Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amehimiza kumfunguza ni yule mfungaji ambaye ni masikini, mgeni nchini au ni yule ambaye tunamwalika katika futari nyumbani kwetu kama mgeni katika ndugu na jamaa? Je, tunapata thawabu kwa kuwakaribisha futari wafungaji ambao tunawaalika mwaliko maalum ndani ya Ramadhaan?

Jibu: Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba amesema:

“Yeyote atakayemfuturisha mfungaji basi anapata ujira mfano wake, ingawa hakupungui chochote katika ule ujira wa mfungaji.”

Ameipokea at-Tirmdihiy.

Makusudio ya mfungaji hapa ni mfungaji katika waislamu na khaswa ambaye anastahiki kupewa swadaqah kwa kulishwa kama mfano wa fakiri, masikini na msafiri. Maana hii ni mfano wa maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yeyote atakayeandaa vita katika njia ya Allaah, basi amepigana vita.”

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

Swaalih al-Fawzaan

´Abdul-´Aziyz Aalish-Shaykh

Bakr Abu Zayd

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (09/34) nr. (17790)
  • Imechapishwa: 24/04/2022