Swali: Hadiyth inayosema:
“Anayesoma Aayat-ul-Kursiy baada ya kila swalah, basi hakuna kizuizi kati yake na kuingia Peponi isipokuwa kifo.”
Jibu: Haina neno. Kumepokelewa njia zingine zinazoitia nguvu ambapo baadhi ni nzuri. Inapendeza kuisoma baada ya swalah. Baada ya mtu kuleta Dhikr asome Aayat-ul-Kursiy. Ni miongoni mwa sababu za kuingia Peponi kwa yule ambaye hakufa juu ya dhambi kubwa. Ambaye amekufa juu ya dhambi kubwa kuna matishio juu yake kwa hali yoyote. Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Swalah tano, ijumaa moja mpaka nyingine na Ramadhaan mpaka Ramadhaan nyingine ni vyenye kufuta yaliyo kati yake midhali mtu atajiepusha na madhambi makubwa.”[1]
Allaah (Ta´ala) amesema:
إِن تَجْتَنِبُوا كَبَائِرَ مَا تُنْهَوْنَ عَنْهُ نُكَفِّرْ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَنُدْخِلْكُم مُّدْخَلًا كَرِيمًا
“Mkijiepusha madhambi makubwa mnayokatazwa Tutakufutieni madhambi yenu madogo na Tutakuingizeni katika mahali patukufu.”[2]
Ameweka sharti ya kujiepusha na madhambi makubwa ili mtu asamehewe na kuingia Peponi.
Kwa hivyo ni wajibu mtu kujiepusha na maasi na asife juu ya dhambi hali ya kuiendeleza. Tunamuomba Allaah atulinde na atusalimishe sote.
[1] Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (994).
[2] 04:31
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23009/ما-صحة-فضل-اية-الكرسي-بعد-كل-صلاة
- Imechapishwa: 08/10/2023
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)