Swali: Washirikina katika ushirikina wao Allaah amewasifu katika Kitabu Chake kuwa wanayafuata yasiyo wazi. Wanazuoni wengi siku hizi wanasema kuwa mtu hakufuru mpaka shubuha iondolewe kwake.

Jibu: Ikiwa kuna shubuha, basi iondolewe kwake shubuha hiyo. Lakini asiyekuwa na shubuha, basi ni vyema na huyo hana udhuru. Akizungumza kwa simu, ataondokewa na shubuha. Akazungumza kwa uwakilishi au kwa barua, ataondokewa na shubuha. Lakini akizungumza na maiti, huyo hana shubuha. Huo ndio ushirikina wa washirikina. Kusema na maiti na kuomba msaada kwake hakuna shubuha hapo, huo ni ushirikina wa wazi wa washirikina waliokuwa wakimuomba al-Laat, al-´Uzza, Manaat na mfano wao. Aidha walikuwa wakiomba Malaika na majini. Huo ndio ushirikina wao. Yule mwenye shubuha huondolewa shubuha hiyo. Kuwaomba msaada majini, Malaika, wasiokuwepo na kuwaomba wafu, si kama kumuomba aliye hai na aliye mbele yako. Kumomba aliye hai na aliye mbele yako, waislamu wote wamekubaliana kuwa hakuna tatizo, kama kumwambia aliye hai  na aliye mbele yako akufanyie uombezi, akuombee kwa Allaah, nikopeshe kitu fulani na fikisha salamu yangu kwa fulani.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31464/ما-حكم-من-يتبعون-المتشابه-في-امور-شركية
  • Imechapishwa: 26/10/2025