Kigezo cha kumsimamishia hoja mzushi na mjinga

Swali: Baadhi ya watu wa zama hizi wamesema kwamba kafiri anayesema au kutenda ukafiri hawi kafiri mpaka hoja isimamishwe dhidi yake na wamewahusisha waabudia makaburi katika hilo?

Jibu: Hayo ni miongoni mwa ujinga wao. Waabudu makaburi ni makafiri, mayahudi ni makafiri na manaswara ni makafiri. Lakini wakati wa kuuliwa, kwanza wanaombwa kutubia; wakitubia ni vyema. Vinginevyo wanauliwa.

Swali: Vipi kuhusu suala la kusimamisha hoja?

Jibu: Wamefikiwa na Qur-aan:

هَـٰذَا بَلَاغٌ لِّلنَّاسِ وَلِيُنذَرُوا بِهِ

“Hii ni ufikishwaji wa ujumbe kwa watu na ili wawaonye kwayo.”[1]

Qur-aan imewafikia na wanaishi kati ya waislamu:

وَأُوحِيَ إِلَيَّ هَـٰذَا الْقُرْآنُ لِأُنذِرَكُم بِهِ وَمَن بَلَغَ

“Nimefunuliwa Wahy hii Qur-aan ili nikuonyeni kwayo na kila itakayomfikia.”[2]

هَـٰذَا بَلَاغٌ لِّلنَّاسِ

“Hii ni ufikishwaji wa ujumbe kwa watu.”

يَا أَيُّهَا الرَّسُولُ بَلِّغْ مَا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ

”Ee Mtume! Fikisha yale yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Mola wako.”[3]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewafikishia, Qur-aan imewafikia na wao wako baina yetu na wanaisikia kupitia redio na njia nyingine. Hata hivyo hawajali. Anapokuja mtu kuwatahadharisha na kuwakataza humdhuru.

[1] 14:52

[2] 6:19

[3] 05:67

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31463/ما-ضابط-قيام-الحجة-على-الجاهل-والمبتدع
  • Imechapishwa: 26/10/2025