Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kufanya jimaa hali ya kusahau kuwa yuko katika mchana wa Ramadhaan?

Jibu: Allaah ndiye mjuzi zaidi kama kweli amesahau kuwa ni Ramadhaan. Ikiwa kweli amesahau basi anayo hukumu ya msahaulifu ambayo ni kutohitaji kulipa. Lakini sidhani kama mtu anasahau kuwa yuko katika mwezi usiokuwa wa Ramadhaan. Labda katika ile siku ya kwanza ya Ramadhaan pengine kweli mtu akasahau. Lakini hata yeye akisahau mke pia atasahau? Kuhusu kutoa kafara kunamlazimu.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaaih wa Naswaaih, uk. 81
  • Imechapishwa: 18/03/2024