Swali: Usiku wa leo tumesikia mizinga zaidi ya mara moja ambapo tukapatwa na shaka kuwa ni ´Iyd au bado ni Ramadhaan. Tumesubiri tusikie kitu kutoka kwa imamu wakati wa Fajr na hatujasikia chochote. Ni ipi hukumu ya kutilia shaka nia katika kufunga au kufungua?
Jibu: Ni wajibu kwa mtu kuhakikisha. Msingi ni kubaki yaliyokuwa vile yalivyokuwa. Endapo kungelikuwa jambo basi lingedhihiri kwa namna ya kwamba watu wangelibainishiwa ili wasile daku na kufunga. Kwa hali yoyote ni kwamba siku hiyo inazingatiwa bado ni Ramadhaan. Kama mwezi ungelikuwa umemalizika basi jambo lingebainika. Katika hali hiyo ni wajibu kwa mtu kufunga kuendelea kufunga bila ya kutia shaka. Kwa sababu msingi ni kubaki kwa Ramadhaan. Ikibainika baada ya siku hiyo kwamba ni ´Iyd, basi atafungua.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/182-183)
- Imechapishwa: 15/05/2026
Swali: Usiku wa leo tumesikia mizinga zaidi ya mara moja ambapo tukapatwa na shaka kuwa ni ´Iyd au bado ni Ramadhaan. Tumesubiri tusikie kitu kutoka kwa imamu wakati wa Fajr na hatujasikia chochote. Ni ipi hukumu ya kutilia shaka nia katika kufunga au kufungua?
Jibu: Ni wajibu kwa mtu kuhakikisha. Msingi ni kubaki yaliyokuwa vile yalivyokuwa. Endapo kungelikuwa jambo basi lingedhihiri kwa namna ya kwamba watu wangelibainishiwa ili wasile daku na kufunga. Kwa hali yoyote ni kwamba siku hiyo inazingatiwa bado ni Ramadhaan. Kama mwezi ungelikuwa umemalizika basi jambo lingebainika. Katika hali hiyo ni wajibu kwa mtu kufunga kuendelea kufunga bila ya kutia shaka. Kwa sababu msingi ni kubaki kwa Ramadhaan. Ikibainika baada ya siku hiyo kwamba ni ´Iyd, basi atafungua.
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/182-183)
Imechapishwa: 15/05/2026
https://firqatunnajia.com/endelea-kufunga-mpaka-kubainike-kinyume-chake/