Swali: Ni ipi hukumu ya mtu ambaye anakesha usiku na anaswali Fajr baada ya kumalizika kwa wakati wake? Je, swalah yake inakubaliwa? Ni ipi hukumu ya swalah zake zingine ambazo anaziswali ndani ya wakati?
Jibu: Ikiwa anakesha usiku na akakosa Fajr ilihali anao uwezo wa kuswali ndani ya wakati – kwa sababu anaweza kulala mapema – na akaswali baada ya kutoka kwa wakati, basi swalah yake hii haikubaliwi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Yeyote atakayefanya kitendo kisichokuwa ndani yake amri yetu atarudishiwa mwenyewe.”[1]
Yule ambaye anaswali swalah nje ya wakati wake pasi na udhuru basi hakika ametenda kitendo kisichoafikiana na amri ya Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), na kwa ajili hiyo anarudishiwa mwenyewe. Pengine mtu huyu akajengea hoja maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Yule mwenye kupitikiwa na usingizi au akaisahau swalah, basi aiswali pale atapoikumbuka. Haina kafara nyingine isipokuwa hiyo.”[2]
Jawabu ni kwamba ambaye anaweza kulala mapema basi anatakiwa kulala mapema. Yule ambaye anaweza kuweka alamu ya kumwamsha basi anatakiwa kufanya hivo. Yule ambaye anaweza kumwomba mtu amwamshe basi anatakiwa kufanya hivo. Kuchelewesha swalah na kuamka nje ya wakati wake kunazingatiwa ni kukusudia kuichelewesha nje ya wakati wake na hivyo haikubaliwi kwake. Kuhusu swalah zake nyenginezo ambazo anaziswali ndani ya wakati zinazingatiwa ni zenye kukubaliwa.
Katika mnasaba huu natumia fursa ya kusema kwamba ni wajibu kwa muislamu kumwabudu Allaah kwa njia inayomridhisha Yeye (´Azza wa Jall). Kwa sababu ameumbwa hapa ulimwenguni kwa lengo la kumwabudu Allaah, na hajui ni lini yatamchukua mauti na hivyo ghafla achukuliwe kutoka ulimwenguni na kupelekwa huko Aakhirah ambapo hakuna malipo. Kama alivosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Anapofariki mwanadamu basi matendo yake hukatika isipokuwa mambo matatu; swadaqah yenye kuendelea, elimu ambayo watu wananufaika nayo au mtoto mwema mwenye kumuombea du´aa.”[3]
[1] Muslim (1718).
[2] al-Bukhaariy (597) na Muslim (684).
[3] Muslim (1631).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/21-22)
- Imechapishwa: 14/05/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/21-22)
Imechapishwa: 14/05/2026
https://firqatunnajia.com/anakesha-nyusiku-na-kukosa-fajr/