Du´aa ya Qunuut haiombwi wakati wa majanga

Swali: Du´aa:

اللهم اهدني فيمن هديت

“Ee Allaah, niongoze miongoni mwa uliowaongoza.”

Je, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifanya Qnuut kwa du´aa hii?

Jibu: Hapana, hakufanya. Mtume alikuwa akifanya Qunuut kwa ajili ya kuwaombea shari iwashukie watu fulani au kuwatakia kheri watu fulani. Ama du´aa hii Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimfundisha al-Hasan ili aitumie katika Qunuut. Kisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa akiswali akiwa imamu, hakuwa akisema kwa njia ya umoja, bali alikuwa akitumia njia ya wingi anapowaombea waislamu, kwa mfano anasema:

اهدني، واغفر لي

”Niongoze, nisamehe.”

Hapo ni pale anapokuwa peke yake. Lakini anapokuwa ndani ya swalah yake anajiombea mwenyewe baina yake na Mola wake. Kama alivyokuwa anasema kwenye sujuud:

اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي ذَنْبِي كُلَّهُ: دِقَّهُ وَجِلَّهُ، وَأَوَّلَهُ وَآخِرَهُ، وَعَلاَنِيَّتَهُ وَسِرَّهُ

“Ee Allaah! Nisamehe dhambi zangu zote; ndogo na kubwa, za mwanzo na za mwisho, za dhahiri na za kujificha.”[1]

Lakini du´aa za jumla katika Khutbah na katika Qunuut huwa ni za pamoja kama:

اللهم اغفر لنا، اللهم ارحمنا، اللهم أنجنا، اللهم انصرنا

“Ee Allaah, tusamehe! Ee Allaah, turehemu! Ee Allaah, tuokoe! Ee Allaah,  tunusuru!”

na mfano wa hayo.

[1] Muslim (482).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31472/هل-ثبت-دعاء-قنوت-الوتر-في-السنة
  • Imechapishwa: 27/10/2025