85 – ´Abdullaah bin ´Amr bin al-´Aasw (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia kuwa amemsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Mtapomsikia muadhini basi semeni kama anavosema, kisha niswalieni. Kwani hakika mwenye kuniswalia mara moja, basi Allaah atamsifu mara kumi. Kisha niombeeni kwa Allaah Njia (الوسيلة),  hakika hiyo ni ngazi Peponi. Haimstahikii isipokuwa mja miongoni mwa waja wa Allaah na nataraji mimi ndiye mwenye kuistahiki. Kwa hivyo mwenye kuniombea kwa Allaah Njia basi utamstahikia uombezi wangu.”[1]

Ameipokea Muslim.

86 – Jaabir  bin ´Abdillaah (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule atakayesema wakati anaposikia adhaana:

اللَّهُمَّ ربَّ هَذه الدَّعْوَةِ التَّامَّةِ والصَّلاَةِ الْقَائِمَةِ آتِ مُحَمَّداً الوسيلة والْفَضِيلَةَ وَابْعَثْهُ مَقَاماً محموداً الذي وَعَدْتَهُ

“Ee Allaah, Mola wa mwito huu uliotimia na swalah iliosimama! Mpe Muhammad Njia (الوسيلة) na fadhilah, na mfikishe daraja yenye kusifiwa ambayo umemuahidi.”

basi utamthubutikia uombezi wangu siku ya Qiyaamah.”[2]

Ameipokea al-Bukhaariy.

MAELEZO

Ndani ya Hadiyth hizi mbili kuna du´aa hii baada ya adhaana na kwamba ambaye atasema hivo basi utamthubutikia uombezi ikiwa ni miongoni mwa watu wanaomwabudu Allaah pekee. Akiwa ni miongoni mwa wapwekeshaji na akasema du´aa hii basi utamstahikia uombezi. Kumepokelewa ziada kwa Muslim inayosema ya kwamba anatakiwa kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baada ya adhaana. Kwa hivyo anatakiwa kuanza kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kisha baada ya hapo ndio aseme du´aa hii.

[1] Muslim (384).

[2] al-Bukhaariy (614).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 89
  • Imechapishwa: 28/10/2025