87 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza: “Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baada ya kuleta Takbiyr alikuwa akinyamaza kitambo kidogo kabla ya kuanza kusoma. Nikasema: “Ee Mtume wa Allaah, namtoa fidia baba yangu na mama yangu kwa ajili yako, nimeona kunyamaza kwako baina ya Takbiyr na kisomo, nini unachosema?” Akasema:

اللَّهُمَّ بَاعِدْ بَيْنِي وَبَيْنَ خَطَايَايَ كَمَا بَاعَدْتَ بَيْنَ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ، اللَّهُمَّ نَقِّنِي مِنْ خَطَايَايَ كَمَا يُنَقَّى الثَّوْبُ الْأَبْيَضُ مِنَ الدَّنَسِ، اللَّهُمَّ اغْسِلْني مِنْ خَطَايَايَ، بِالثَّلْجِ وَالْماءِ وَالْبَرَدِ

“Ee Allaah! Niweke mbali mimi na makosa/dhambi zangu kama ulivyoweka mbali baina ya mashariki na magharibi. Ee Allaah! Nitakase na makosa/dhambi zangu kama Unavyoitakasa nguo nyeupe na uchafu. Ee Allaah! Nisafishe na makosa/dhambi zangu kwa theluji, kwa maji na kwa barafu.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

MAELEZO

Hadiyth hii ndio sahihi na bora zaidi katika zile namna zilizopokelewa katika du´aa za kufungulia swalah. Mashaykh wawili, al-Bukhaariy na Muslim, wameafikiana juu yake. Matamshi ya du´aa hii tayari yamekwishatolewa maelezo[2].

[1] al-Bukhaariy (744) na Muslim (598).

[2] Maana yake imekwishatangulia katika Hadiyth (51).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 90
  • Imechapishwa: 28/10/2025