88 – ´Ubaadah amesimulia kuwa ´Umar alikuwa akisoma kwa sauti maneno haya na akisema:

سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ وَبِحَمْدِكَ وتَبَارَكَ اسْمُكَ وَتَعَالى جَدُّكَ وَلا إِله غَيْرُكَ

“Kutakasika ni Kwako, ee Allaah, kutokamana na kasoro zote na himdi zote ni Zako. Limetukuka jina Lako, ufalme Wako ni mkubwa na hapana mungu wa haki mwengine asiyekuwa Wewe.”[1]

Ameipokea Muslim.

MAELEZO

Hii ndio du´aa fupi zaidi miongoni mwa zile du´aa zilizopokelewa za kufungulia swalah. Ndio du´aa bora zaidi yenyewe kama yenyewe, kwa sababu inamtakasa na kumsifu Allaah[2]. ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) alikuwa akiwalakinisha nayo juu ya mimbari ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Maana ya:

سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ

“Kutakasika ni Kwako, ee Allaah… ”

Ni kumtakasa Allaah (Subhaanah). Kwa maana nyingine ni kuwa tunakutakasa, tunakutukuza na tunakutenga mbali kutokana na mapungufu na kasoro. Matakosa yanayolingana Nawe, ee Allaah.

Maana ya:

وَبِحَمْدِكَ

“… na himdi zote ni Zako.”

Bi maana nakusanya, licha ya kukutakasa, kukuhimidi na kukusifu kuliko kamilika.

Maana ya:

وتَبَارَكَ اسْمُكَ

“Limetukuka jina Lako… “

Inatokana na baraka. Maana yake ni kwamba baraka hufikiwa kwa kutajwa Kwako. Au pia kwamba limetukuka na kutakasika jina Lako, kwani ni Jina tukufu.

Maana ya:

وَتَعَالى جَدُّكَ

”… ufalme Wako ni mkubwa.”

Bi maana utukufu na shani Yako ni kubwa. Umekuwa mkubwa na kutukuka. Utukufu (الجد) lina maana nyingi. Hapa maana yake ni utukufu (العظمة)[3].

Maana ya:

وَلا إِله غَيْرُكَ

“Hapana mungu mwengine asiyekuwa Wewe.”

Bi maana mwabudiwa. Maana yake ni kwamba hakuna mwabudiwa mwingine wa haki asiyekuwa Wewe.

[1] Muslim (399).

[2] Tazama maana yake ”Majmuu´-ul-Fataawaa” (22/294).

[3] Tazama ”Lisaan-un-´Arab” (03/108) na ”an-Nihaayah” (01/244).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 90-91
  • Imechapishwa: 28/10/2025