89 – ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anaposimama kuswali husema:

وَجَّهْتُ وَجْهِي للَّذِي فَطرَ السَّمَواتِ والأَرْضَ حَنيفاً وَما أَنا مِنَ الْمُشْرِكِينَ إِنَّ صَلاَتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي للهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ لاَ شَرِيكَ لَهُ وَبِذَلِكَ أُمِرْتُ وَأَنَا مِنَ الْمُسْلِمِينَ اللَّهُمَّ أَنْتَ الْمَلِكُ لاَ إِلهَ إِلاَّ أَنْتَ رَبِّي وَأَنَا عَبْدُكَ ظَلَمْتُ نَفْسِي واعْتَرَفْتُ بِذَنْبِي فَاغْفِرْ لِي ذُنُوبِي جَمِيعاً فإِنَّهُ لاَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلاَّ أَنْتَ واهْدِنِي لأَحْسَنَ الأَخْلاَقِ لاَ يَهْدِي لأَحْسَنِهَا إِلاَّ أَنْتَ واصْرِفْ عَنِّي سَيِّئَها لاَ يَصْرِفُ عَني سَيِّئَهَا إِلاَّ أَنْتَ لَبَّيْك وَسَعْدَيْكَ والْخَيْرُ كُلُّهُ في يَدَيْكَ وَالشَّرُّ لَيْسَ إِلَيْكَ أَنا بِكَ وإِلَيْكَ تَبَارَكْتَ وَتَعَالَيْتَ أَسْتَغْفِرُكَ وأَتُوبُ إِلَيْكَ

“Nimeuelekeza uso wangu kwa yule ambaye Ameumba mbingu na ardhi, hali ya kumtakasia Yeye dini yangu na sikuwa mimi ni katika washirikina. Hakika swalah yangu, kichinjwa changu, uhai wangu na kufa kwangu ni kwa Allaah, Mola wa walimwengu, Yeye asiyekuwa na mshirika; kwa hilo nimeamrishwa na mimi ni katika Waislamu. Ee Allaah! Wewe ndiye Mfalme. Hapana mola mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Wewe. Wewe ndiye Mola Wangu na mimi ni mja Wako. Nimeidhulumu nafsi yangu. Nimekiri madhambi yangu. Nisamehe madhambi yangu yote. Hakika hakuna mwengine asamehae madhambi isipokuwa Wewe. Niongoze katika tabia njema. Hakuna aongozae katika tabia nzuri isipokuwa Wewe. Niepushe na tabia mbaya. Hakuna mwengine mwenye kuepusha na tabia mbaya isipokuwa Wewe. Naitikia mwito Wako na kufuata maamrisho Yako. Kheri zote ziko mikononi Mwako. Shari haitoki Kwako. Nimepatikana kwa ajili Yako na ni Wako. Umetakasika na umetukuka. Nakuomba msamaha na ninarejea Kwako.”[1]

Ameipokea Muslim.

MAELEZO

Hii ndio du´aa ndefu ya kufungulia swalah katika swalah inayopendeza, kama ilivyo katika upokezi wa an-Nasaa´iy kupitia kwa Muhammad bin Maslamah ambaye ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anaposimama huswali swalah ya kujitolea[2]. Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Nami ni miongoni mwa waislamu.”

Imekuja katika tamko jengine:

“Nami ndiye muislamu wa kwanza.”

Kwa sababu yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye muislamu wa kwanza wa ummah huu. Lakini muislamu anapofungua swalah yake aseme:

“Nami ni miongoni mwa waislamu.”

[1] Muslim (771).

[2] an-Nasaa´iy (898).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 92-93
  • Imechapishwa: 28/10/2025