Du´aa ya kukhitimisha Qur-aan katika Tarawiyh ni Bid´ah?

Swali: Baadhi ya watu wanawakemea maimamu wa misikiti ambao wanasoma du´aa ya kukhitimisha Qur-aan katika mwezi wa Ramadhaan na wanasema kuwa haijathibiti kutoka kwa yeyote katika Salaf. Ni upi usahihi wa hilo?

Jibu: Hapana neno katika hilo. Imethibiti kutoka kwa baadhi ya Salaf kwamba wamefanya hivo. Isitoshe ni du´aa ambayo sababu yake imepatikana ndani ya swalah na hivyo inajumuishwa na du´aa za swalah kama vile Qunuut na wakati wa majanga.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/32)
  • Imechapishwa: 10/04/2023