Swali: Wakati mswaliji anajiunga na swalah baada ya kupitwa sehemu ya swalah aombe du´aa ya kufungulia? Je, kuna tofauti kati ya Rukuu´ na hali nyingine?
Jibu: Hali inatofautiana kutegemea na ile hali ya huyo ambaye amekuja kuchelewa. Ikiwa amepitwa tu na ile Takbiyr ya kwanza na ana uwezo wa kukusanya kati ya du´aa ya kufungulia swalah na kisomo cha al-Faatihah afanye hivo. Vinginevyo atatosheka na kile kinachomuwezekea katika kusoma al-Faatihah. Kwa hayo litafahamika jibu kwa yaliyobaki. Kwa kufupisha ni kwamba amfuate imamu. Asisimame huku anaomba du´aa ilihali imamu amekwishasujudu au amekwisharukuu. Bali asujudu au kurukuu pamoja naye.
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sa-altu Abiy, uk. 149
- Imechapishwa: 03/07/2022
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket