Du´aa moja kwa moja baada ya kumalizika swalah

Swali: Baadhi ya watu punde tu baada ya kumalizika swalah ya faradhi wanaomba du´aa na wala hawasomi Adhkaar.

Jibu: Wafunzwe Sunnah. Sunnah ni kusoma Dhikr zilizopokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kuomba du´aa kwa pamoja kwa njia ya kunyanyua sauti wakati wa kuomba du´aa kwa pamoja ni jambo linapingana na Sunnah. Bali ni Bid´ah. Ima mtu amtaje Allaah peke yake au amtaje Allaah ndani ya nafsi yake kwa mujibu wa vile ilivyotajwa katika Shari´ah kama mlivosikia.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22574/حكم-من-يشرعون-في-الدعاء-عقب-الفريضة
  • Imechapishwa: 04/07/2023