Du´aa mbaya kwa muislamu anayeenda kinyume na Shari´ah

Swali: Hadiyth ya Salamah bin Akwa´ ya yule bwana aliyekula mbele ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa kutumia mkono wa kushoto ambapo akamwambia: ”Kula kwa mkono wa kulia.” Bwana yule akajibu kuwa hawezi. Akamwambia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): ”Hutoweza. Hakuna kichomzuia isipokuwa kufanya kiburi.” Je, hapa kunachumwa faida ya kufaa kumuombea du´aa mbaya muislamu anapoenda kinyume na amri ya Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Kinachodhihiri katika Hadiyth ni kufaa itapojulikana kuwa amefanya jeuri. Lakini kusamehe ndio bora zaidi. Kumsamehe na kumuombea du´aa nduguyo ndio bora zaidi kama ilivyopokelewa katika maandiko mengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22348/ما-حكم-الدعاء-على-المسلم-اذا-خالف-الشرع
  • Imechapishwa: 17/02/2023