Du´aa iliyokusanya na yenye manufaa

Allaah (Ta´ala) amesema:

اهْدِنَا الصِّرَاطَ الْمُسْتَقِيمَ

”Tuongoze katika njia ilionyooka.”

Bi maana tuongoze, tuelekeze na tuwafikishe katika njia ilionyooka. Nayo ni ile njia ya wazi inayomfikisha mtu kwa Allaah na kwenye Pepo Yake. Ni kule kuijua haki na kuitendea kazi. Tuongoze kuielekea njia na tuongoze kwenye njia. Kuongozwa kwenye njia ni kule kulazimiana na Uislamu na kujiepusha na dini nyenginezo. Kuongozwa katika njia kunakusanya uongofu kwa mkusanyiko wa mambo ya dini kwa kuyajua na kuyatendea kazi.

Du´aa hii ni miongoni mwa du´aa zilizokusanya na zenye kumnufaisha mja. Kwa ajili hiyo ndio maana ikawa ni lazima kwa mtu kuiomba katika kila Rak´ah ya swalah yake kutokana na kuhitajia kwake jambo hilo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Taysiyr-ul-Kariym, sid. 27
  • Imechapishwa: 02/05/2020