Du´aa hii inasomwa pia baada ya swalah zinazopendeza

Swali: Anayeswali Rak´ah mbili zinazopendeza na akamtaja Allaah kwa kusema:

أستغفر الله، أستغفر الله، أستغفر الله، اللهم أنت السلام، ومنك السلام، تباركت يا ذا الجلال والإكرام

”Namuomba Allaah msamaha. Namuomba Allaah msamaha. Namuomba Allaah msamaha. Ee Allaah! Hakika wewe ndiye as-Salaam. Amani inatoka Kwako. umebarikika, Ee Mwenye utukufu na ukarimu.”

Jibu: Hivo ndio Sunnah.

Swali: Hata swalah inayopendeza pia?

Jibu: Swalah yoyote.

Swali: Au katika Dhuhr au wakati wowote?

Jibu: Ndio. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anapomaliza kuswali husema:

أستغفر الله، أستغفر الله، أستغفر الله، اللهم أنت السلام، ومنك السلام، تباركت يا ذا الجلال والإكرام

”Namuomba Allaah msamaha. Namuomba Allaah msamaha. Namuomba Allaah msamaha. Ee Allaah! Hakika wewe ndiye as-Salaam. Amani inatoka Kwako. umebarikika, Ee Mwenye utukufu na ukarimu.”

Msingi ni kwamba swalah inayopendeza ni kama swalah ya faradhi katika hili. Isipokuwa kwa dalili inayoonyesha kinyume chake. Dalili ya hilo ni:

“Swalini kama mlivyoniona nikiswali.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23349/هل-الاذكار-دبر-الصلوات-تشمل-النوافل
  • Imechapishwa: 31/12/2023