Akianza swalah kwa kuelekea Qiblah ndio salama zaidi

Swali: Hadiyth ya Anas (Radhiya Allaahu ´anh) anayesimulia:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anapotaka kuswali swalah ya kujitolea basi huelekea Qiblah na akaleta Takbiyr kisha akaelekea kule ambako mnyam umeelekea.”

Je, kuelekea Qiblah ni kwa njia ya uwajibu?

Jibu: Hadiyth ya Anas ameipokea al-Bukhaariy na Muslim kupitia njia nyingi ya kwamba alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiswali kule kipando kinapoelekea anapokuwa safarini. Akifanya yale yanayofahamishwa na Hadiyth ya Anas ambapo akaianza swalah kwa kuelekea Qiblah ndio kushika tahadhari zaidi. Huko ni kwa njia ya kuichunga Sunnah na kwa njia ya usalama zaidi. Vinginevyo Hadiyth nyenginezo zote zilizopokelewa na al-Bukhaariy na Muslim haikutaja jambo la kuianza swalah kwa kuelekea Qiblah. Humo imetajwa tu ya kwamba alikuwa akiswali kule mnyama ulipoelekea.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23347/حكم-استقبال-القبلة-في-النافلة-على-الراحلة
  • Imechapishwa: 31/12/2023