Swali: Ni vipi mtoto atapigiwa Takbiyr za swalah ya jeneza?

Jibu: Mtoto ataswaliwa kama mtu mzima, atapigiwa Takbiyr nne. Katika du´aa ya mwisho baada ya Takbiyr ya tatu, baada ya kusema:

اللهم اغفر لحينا وميتنا، وشاهدنا وغائبنا، وصغيرنا وكبيرنا، وذكرنا وأنثانا، اللهم من أحييته منا فأحيه على الاسلام، ومن توفيته منا فتوفه على الايمان

“Ee Allaah! Msamehe aliyehai katika sisi na aliyekufa katika sisi, aliyepo na asiyekuwepo, wadogo wetu na wakubwa wetu, wakiume wetu na wakike wetu. Ee Allaah! Ambaye utampa uhai katika sisi basi mpe uhai katika Uislamu na utayemfisha katika sisi basi mfishe juu ya imani.”

Aseme baada yake:

اللهم اجعله ذخرًا لوالديه، وفرطًا وشفيعًا مجابا، اللهم أعظم به أجورهما، وثقل به موازينهما، وألحقه بصالح سلف المؤمنين، واجعله في كفالة إبراهيم عليه الصلاة والسلام، وقه برحمتك عذاب الجحيم

“Ee Allaah! Mjaalie awe ni mtangulizi, ujira, muombezi anayekubaliwa kwa ajili ya wazazi wake. Ee Allaah! Ifanye mizani yao iwe mizito na ukuze ujira wao kupitia mtoto huyu. Vilevile muunganishe na waumini wema waliotangulia na umjaalie awe katika ulinzi wa Ibraahiym (´alayhis-Swalaatu was-Sallaam) na umkinge kwa huruma Wako kutokamana na adhabu ya Moto.”

Hii ni du´aa ya jumla. Hii ndiyo iliyopokelewa kuhusu mtoto.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31241/كيف-يكون-الدعاء-في-جنازة-الصغير
  • Imechapishwa: 17/10/2025