Kuinua sauti wakati wa du´aa kwa lengo la kuwafunza watu Sunnah

Swali: Je, ni jambo limewekwa katika Shari´ah kuinua sauti katika du´aa kwa ajili ya kuwafundisha watu kama alivyofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Akiinua sauti katika baadhi ya nyakati kwa ajili ya kufundisha hakuna tatizo. Akipandisha sauti yake katika kufundisha ili watu wajifunze du´aa, hilo ni jambo zuri. Ni kwa minajili ya kufunza. Ibn ´Abbaas aliinua sauti yake katika kusoma akasema:

“Ili mjue kuwa hiyo ni Sunnah.”

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31240/هل-يشرع-رفع-الصوت-بالدعاء-لتعليم-الناس
  • Imechapishwa: 17/10/2025