Kurefusha du´aa baada ya kumaliza Qur-aan

Swali: Kuhusu kurefusha du´aa ya kumalizia Qur-aan ambapo mtu anafanya saa nzima au saa kasoro robo – je, hili limekubaliwa?

Jibu: Kujitahidi katika du´aa na kuzidisha du´aa yote ni jambo jema. Omba du´aa kwa wingi, kwani Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Hakuna mja anayemwomba Allaah du´aa ambayo haina dhambi wala kukata udugu isipokuwa Allaah humjibu kwa mojawapo ya mambo matatu: ima kumharakishia du´aa yake duniani, kumhifadhia nayo kwa ajili ya Aakhirah au kumkinga na shari mfano wake.” Wakasema: ”Ee Mtume wa Allaah, basi tufanye kwa wingi?” Akasema: ”Allaah ndiye zaidi.”

Kwa hiyo Allaah kufanya du´aa kwa wingi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31245/ما-حكم-الاطالة-في-دعاء-ختم-القران
  • Imechapishwa: 17/10/2025