Ibn Baaz akizungumzia usahihi wa Hadiyth ya Basmalah kabla ya wudhuu´

Swali: Hadiyth ya kusema Basmalah wakati wa wudhuu´ njia zake zote ni dhaifu?

Jibu: Lakini baadhi ya wanazuoni wamezifanya kuwa ni nzuri, kwa msemo mwingine ni kwamba zinasapotiwa na nyenginezo. Mfano wa wanazuoni hao ni pamoja na Ibn-us-Swalaah na Ibn Kathiyr katika tafsiri yake ya Qur-aan ambaye amesema kuwa ni nzuri alipokuwa akifasiri Suurah ”al-Maa-idah”.

Swali: Hadiyth inazingatiwa kuwa ni nzuri hata kama ina udhaifu mkubwa licha ya njia zake nyingi?

Ibn Baaz: Hapana, udhaifu mkali hauifanya Hadiyth kuwa nzuri.

Swali: Je, njia mbili zinatosha?

Ibn Baaz: Njia mbili au zaidi ya hizo. Ikiwa udhaifu ni mwepesi, basi Hadiyth inakuwa nzuri kwa kusapotiwa na nyenginezo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31257/هل-يتحسن-الحديث-الضعيف-بتعدد-الطرق
  • Imechapishwa: 17/10/2025