Ni ipi tofauti kati ya sharti ya al-Bukhaariy na sharti ya al-Bukhaariy na Muslim?

Swali: Ni ipi tofauti kati kwa mujibu wa sharti ya al-Bukhaariy na kwa mujibu wa sharti ya al-Bukhaariy na Muslim?

Jibu: Kama ulivyosikia. Sharti ya al-Bukhaariy ni yenye nguvu zaidi kwa upande wa uangalifu katika uhifadhi na kuungana kwa cheni.

Swali: Je, sharti ya al-Bukhaariy na Muslim inajumuishwa ndani ya sharti ya al-Bukhaariy?

Jibu: Lakini kuna tofauti kati ya hayo mawili. Ikiwa ni sharti ya al-Bukhaariy peke yake, basi ni yenye nguvu zaidi kuliko ya Muslim. Lakini wakiafikiana, basi sharti zao mbili zinakuwa zimeungana. Wakitofautiana, sharti ya al-Bukhaariy ndio yenye nguvu zaidi kuliko ya Muslim.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31267/ما-الفرق-بين-شرط-البخاري-وشرط-الشيخين
  • Imechapishwa: 17/10/2025