Swali: Je, Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiacha Swalah ya Dhuhaa katika safari?

Jibu: Aliiswali wakati wa utekwaji. Aliingia nyumba ya binadamu yake Umm Haaniy na akaswali Dhuhaa Rakaa nane. Dhuhaa na Swalah za Nawaafil ambazo ni Mutlaq, kama Swalah za usiku na Witr, haziachwi katika safari.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (02) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/muq–14331116.mp3
  • Imechapishwa: 17/06/2015