Swali: Vipi tutaoanisha kutotahadharisha wenye kwenda kinyume na kubainisha njia iliyonyooka kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa ni mwenye kueneza bishara njema na muonyaji? Tukiwanyamazia wenye kwenda kinyume na…

Jibu: Kwnaza wafunze njia iliyonyooka. Watakuja kuwajua wenye kwenda kinyume. Ni jambo lisilokuwa na faida kumtahadharisha mtu asiyekuwa na misingi wala elimu. Linaweza kupelekea katika uadui tu. Wafunze njia iliyonyooka, wafanye waielewe Dini ya Allaah. Kisha baada ya hapo ima wao wenyewe watakuja kufahamu ni nani mwenye kwenda kinyume au wewe unaweza kuwazindua hilo. Hata hivyo si jambo la sawa ukaanza Da´wah kwa kumtukana na kumponda fulani wakati watu hawajui lolote.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (02) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/muq–14331116.mp3
  • Imechapishwa: 17/06/2015