Dereva anayebeba pombe kueneza kwenye makampuni

Swali: Muislamu nje ya nchi ambaye anaswali na kufunga Ramadhaan. Lakini anafanya kazi ya kama dereva wa lori na anabeba pombe kwenda katika makampuni. Ni ipi hukumu ya kazi yake hii kwa sababu wengi katika wateja ni makafiri?

Jibu: Haijuzu kwake kufanya kazi hiyo kama ni muislamu. Haijuzu kwake kubeba pombe. Anaichafua nafsi yake kwa jambo hilo. Yeye ni muislamu. Allaah amemkirimu Uislamu. Milango ya riziki ni mingi. Atafuta riziki yake:

وَمَن يَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ فَهُوَ حَسْبُهُ

“Na yeyote yule atakayemtegemea Allaah, basi Yeye humtosheleza.”[1]

Atafute riziki kwa njia nyingine.

[1] 65:02-03

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (46)
  • Imechapishwa: 14/09/2024