Da´wah ya Muhammad Qutwub katika Tawhiyd inahusiana tu na Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah

6- Mtu amesifia kitabu cha Tawhiyd cha Muhammad Qutwub alichowaandikia wanafunzi wa shule ya sekondari na kusema kuwa humo ametoa yale mambo ya ´Aqiydah kwa njia rahisi.

Muhammad Qutwub katika madhehebu, lakini kitendo ni upungufu mkubwa. Hili ndilo tulilokuwa tunachelea kutokea mtu akikata mahusiano kati yetu sisi na vitabu vya Salaf-us-Swaalih na badala yake akavibadilisha kwa vingine vipya. Kwa kiasi kikubwa kazi ya Muhammad Qutwub (Hafidhwahu Allaah) inahusiana tu na Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah. Ni kitu ambacho kila mtu anakiamini. Jamii nyingi za makafiri wanakiri hili, jambo ambalo Allaah Amelisema kuhusu wao katika Kitabu Chake. Haitoshi. Siyo hiyo ´Aqiydah ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyofikisha na akaita kwayo. Mitume wote walilingania katika Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah ambayo ni kumwabudu Allaah Mmoja na kutomshirikisha Yeye na chochote. Wakati Allaah Anapotaja Aayah zinazozungumzia Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah ni kwa sababu tu ya kuwahoji washirikina na kuthibitisha ni kwa nini Yeye tu ndiye anatakiwa kuabudiwa na sio mwingine. Malengo ya ´Aqiydah sio Tawhiyd-ya-Rubuubiyyah. Vinginevyo Abu Jahl na Abu Lahab wangelikuwa wapwekeshaji kwa sababu walikiri aina hii ya Tawhiyd.

Ni lazima kuelewa, kwamba nguvu zinatakiwa kuwekwa katika Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah na wabainishiwe nayo wanafunzi. Kwa sababu Uislamu wa kweli ndio maana ya Shahaadah na kila kinachopelekea katika ´Aqiydah ya Waislamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Bayaan li Akhtwaa’ Ba´dhw-il-Kuttaab, uk. 24-25
  • Imechapishwa: 23/04/2015