Ahl-us-Sunnah wanawafunza watu Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hawataki kutoka kwao malipo wala shukurani. Hawataki kutoka kwao wachukue kadi za kupigia kura wala wawachague wao. Hawataki kutoka kwao wawape pesa zao. Lakini wanawafunza. Hatukupeni kitu nanyi msitupe kitu. Sisi hatuna chochote cha kuwapeni na sisi hatukuombeni pesa kwa ajili ya kuwalingania. Tunalingania kwa ajili ya kutafuta uso na radhi za Allaah (´Azza wa Jall). Nanasihi ndugu kutoketi katika vikao vya ndugu ´Abdullaah al-Murtadhiy. Msiketi naye. Ana mambo ya shubuha. Yeye mwenyewe anazo shubuha. Vipi utaketi chini ya mtu ambaye yeye mwenyewe kichwa chake kimejaa mambo ya shubuha? Alisoma hapa na alikuwa msitari wa mbele. Alikuwa akiwafunza ndugu zake na mambo yote hayo ya shubuha yalikuwa mbali naye. Sijui ni vipi alipata shubuha hizo.
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: http://muqbel.net/sounds.php?sound_id=20
- Imechapishwa: 10/01/2021
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)