Wale wanaolingania katika Uislamu wanatakiwa kuaza kulingania katika kushuhudia ya kwamba hapana mungu wa kweli isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah kwa kubainisha na kufafanua na si kimatamshi peke yake. Kwa hivyo haijuzu kwetu kuacha mambo ya ki-Fiqh na mambo ya tofuti. Tukifanya hivo maana yake ni kwamba tumeacha pia kulingania katika shahaadah. Ni ipi nukta ya nne?

Muulizaji: Hawakosoi – Jamaa´at-ut-Tabliygh – makundi mengine ya Kiislamu?

al-Albaaniy: Vilevile wanaacha kukosoa makundi mengine ya Kiislamu. Ni kitu gani hicho? Mimi ni Salafiy na wewe ni Khalafiy. Kwa nini hunikosoi? Kwa sababu niko juu ya haki au juu ya batili? Hapana, kwa sababu jambo hilo linafarikisha. Ni ipi basi faida ya Da´wah yako ukiniacha juu ya upotofu wangu? Ni ipi basi faida ya Da´wah yangu nikikuacha juu ya upotofu wako? Ni lazima tutamke neno la haki. Kwani wao hawakusoma katika kitabu ”Hayaat-us-Swahaabah” kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuuasia Abu Dharr nyasia nyingi ikiwa ni pamoja vilevile na kutojali kwa ajili ya Allaah lawama za wenye kulaumu. Huu ni wasia mmoja miongoni mwa nyasia za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa Abu Dharr.

Kwa hivyo ni lazima tusome na tutendee kazi yale tuliyojifunza. Kuziepuka nukta hizi nne maana yake ni kuepuka kushikamana na ule Uislamu aliokuja nao Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (525)
  • Imechapishwa: 22/12/2020