Swali: Ni yapi maoni yako juu ya wingi wa mikusanyiko wa sehemu za starehe za vijana ikiwa malengo ni kwa ajili ya kulingania na kupeana nasaha?

Jibu: Mimi sipendekezi sehemu za starehe. Mimi napendekeza mikusanyiko ya misikitini. Ambaye yuko na jambo zuri la kusema basi na akaliseme na kulieneza msikitini. Akawafunze watu msikitini. Hizi sehemu za starehe, mikusanyiko ya kwenye vyumba na safari ni zenye kuweka utata. Watu wasiofaa wanaenda huko tofauti na msikitini.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Muhadhara: Waswiyyat-un-Nabiy http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/wasiyah%20nabi-21-11-1436-01.mp3
  • Imechapishwa: 17/07/2018