Swali: Ni zipi sifa za mkusanyiko wa waislamu uliotajwa katika Hadiyth ya Hudhayfah (Radhiya Allaahu ´anh): “Unaninasihi nifanye nini nikikutana na hilo?” Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Shikamana na mkusanyiko wa waislamu na kiongozi wao.” Nikasema: “Ikiwa hakutokuwepo mkusanyiko wala kiongozi?” Akasema: “Jiepushe na makundi yote hata kama utahitajia kuuma meno mshina wa mti mpaka ufariki.”?[1]

Jibu: Mkusanyiko wa waislamu ni ule wenye kupita katika njia ya Allaah na njia ya Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wanafuata Qur-aan na Sunnah. Huu ndio mkusanyiko wa waislamu.

[1] al-Bukhaariy (3606) na Muslim (1847).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Muhadhara: Waswiyyat-un-Nabiy http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/wasiyah%20nabi-21-11-1436-01.mp3
  • Imechapishwa: 17/07/2018