Swali: Kuna mwanamke mimba yake ya miezi mitatu imeharibika. Je, damu inayomtoka inahesabiwa kuwa ni nifasi?

Jibu: Ndio. Damu inayomtoka wakati mimba inapoharibika baada ya siku thamanini, bi maana miezi miwili na siku ishirini, ni nifasi ikiwa ni damu inayotoka. Kwa kuwa ameingia ndani ya twahara ambapo mtoto kishakuwa mifupa. Siku arubaini inakuwa tone ya mbegu, arubaini nyingine inakuwa pande la nyama, kisha arubaini nyingine inakuwa mifupa. Hivyo ameingia katika twahara ambapo mtoto kishakuwa mifupa. Arubaini ya tatu kipomoko kinakuwa na hukumu ya mtoto, bi maana kwamba mimba ikiharibika na akatokwa na damu inahesabika kuwa ni nifasi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (43) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-3-29.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020