Swali: Mwenye kukumbuka kuwa hakuswali Dhuhr wakati kunapokiwa swalah ya ´Aswr. Je, aingie pamoja nao kwa nia ya Dhuhr?

Jibu: Hapana, kwa kuwa kupangilia [swalah] ni jambo linawezekana sasa. Aswali Dhuhr kwanza kisha baadae aingie pamoja nao kwa nia ya ´Aswr na akamilishe swalah yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (43) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-3-29.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020