Damu inayochuruzika wakati wa kuchinja

Swali: Damu inayotoka kwenye mnyama wakati wa kuchinja ni safi?

Jibu: Hapana. Chenye kuchuruzika wakati wa kuchinja ni haramu na ni najisi:

قُل لَّا أَجِدُ فِي مَا أُوحِيَ إِلَيَّ مُحَرَّمًا عَلَىٰ طَاعِمٍ يَطْعَمُهُ إِلَّا أَن يَكُونَ مَيْتَةً أَوْ دَمًا مَّسْفُوحًا أَوْ لَحْمَ خِنزِيرٍ فَإِنَّهُ رِجْسٌ أَوْ فِسْقًا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللَّـهِ بِهِ

“Sema: “Sipati katika yale niliyofunuliwa Wahy kwangu kilichoharamishwa kwa mlaji kukila isipokuwa kiwe ni nyamafu [mzoga] au damu inayomwagika au nyama ya nguruwe – kwani hiyo ni uchafu au ufasiki, kimetajiwa ghairi ya Allaah.” (06:145)

Hii ndio damu yenye kuchuruzika. Ama damu inayobaki kwenye nyama ni safi. Ikiingia kwenye nguo zako haziwi najisi kwa sababu ni safi. Ni yenye kusamehewa na inaliwa pamoja na nyama.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (02) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/omdh–14340204.mp3
  • Imechapishwa: 25/08/2020