Mkojo wa paka ni najisi?

Swali: Je, mkojo wa paka ni msafi kwa kuzingatia ya kwamba inaishi na watu?

Jibu: Paka ni safi kwa sababu inaishi pamoja na watu. Lakini mnyama asiyeliwa, basi na mkojo wake pia ni najisi. Haijalishi kitu sawa akiwa ni paka au mnyama mwingine. Mate ya paka ndio masafi. Kile ambacho paka inakula au kunywa ndani yake kinabaki pia kuwa ni kisafi. Mkojo wake ni najisi na unajumuishwa na mikojo mingine.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (02) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/omdh–14340204.mp3
  • Imechapishwa: 25/08/2020