Swali: Je, ni sahihi kuwa kuna Taswawwuf inayofaa? Kuna wanaosema kuwa elimu ya njia na kumfikia Allaah inapatikana katika Qur-aan na Sunnah, lakini Suufiyyah wamezisha mengine kutoka kwao wenyewe. Sisi ni wenye haki zaidi nayo…

Jibu: Elimu ya Qur-aan na Sunnah haiitwi “Taswawwuf”. Inaitwa kuwa ni elimu ya Qur-aan na Sunnah. Kuhusiana na Taswawwuf chimbuko lake ni kuipa nyongo dunia, az-Zuhd. Chimbuko la Taswawwuf lilianza kupetuka mipaka katika kuipa nyongo dunia na ´ibaadah. Hili ndio chimbuko lake. Baada ya hapo ikakua na kufikia upeo wa ukanaMungu na imani ya Wahdat-ul-Wujuud. Hii ndio natija ya mwenye kwenda kinyume na Qur-aan na Sunnah. Haijalishi kitu hata kama mwanzoni wake atakuwa anakusudia kheri.

Lililo la wajibu ni kukomeka kwa Qur-aan na Sunnah. Ndani yake mna ya kutosheleza. ´Ibaadah inakuwa kwa kuafikiana na Qur-aan na Sunnah. Uchaji Allaah unakuwa kwa kuafikiana na Qur-aan na Sunnah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (01) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/muq–14331103.mp3
  • Imechapishwa: 17/06/2015