Hoja na dalili kutoka katika Kitabu cha Allaah, Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), maneno ya Salaf-us-Swaalih wenye kuzingatiwa na maimamu wa uongofu, yote yanabainisha na kuafikiana juu ya kwamba Qur-aan ni maneno ya Allaah na hayakuumbwa na mwenye kusema Qur-aan imeumbwa ni kafiri. Kwa kuwa amekadhibisha Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume wa Allaah na ameenda kinyume na Ijmaa´ ya Salaf-us-Swaalih – Allaah awawie radhi. Maswahabah wamekubaliana juu ya kwamba Qur-aan ni maneno ya Allaah na kadhalika Taabi´uun, mpaka alipokuwa khabithi huyu Jahm bin Swafwaan akamzulia Allaah uongo huu mkubwa kwamba Qur-aan imeumbwa kama ambavyo vilevile alivyozusha uongo wa kuzikanusha Sifa za Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) na kuzipotosha. Hivyo akawa amekanusha kuwepo juu kwa Allaah (al-´Uluw), juu ya mbingu, akakanusha kuwa amelingana juu ya ´Arshi, akakanusha kuwa Allaah anazungumza, akakanusha kwamba Ibraahiym ni Khaliyl wa Allaah, Muusa ni msemezwa wa Allaah na upotevu mwingineo.
- Muhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: adh-Dhariy´ah ilaa Bayaan Maqaaswid Kitaab-ish-Sharï´ah (1/343)
- Imechapishwa: 26/08/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)