Swali: Je, cheo chenye kusifiwa ambacho Allah (´Azza wa Jall) amemwahidi Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kimefupilizika kwa Uombezi?

Jibu: Sahihi ni kwamba cheo chenye kusifika kimeenea na inahusu kila nafasi ambayo watu wanasifiwa kwayo. Katika hayo kunaingia pia Uombezi mkuu. Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam) wataomba udhuru kutokana na jambo hilo mpaka pale itakapomfikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hapo ndipo atafanya uombezi na Allaah (´Azza wa Jall) amkubalie maombezi yake. Kwa hivyo sahihi ni kwamba cheo kinachosifiwa ni chenye kuenea.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/194)
  • Imechapishwa: 26/04/2026