Chakula cha mwisho alichokula Mtume

Abu Ziyaad amesema:

“Nilimuuliza ´Aaishah juu ya kula vitunguu maji. Akasema: “Ndio chakula cha mwisho alichokula Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndani yake kulikuwa na vitunguu maji.”[1]

Hadiyth hii ni geni na cheni ya wapokezi wake ni njema. Ameipokea Ahmad bin Hanbal katika “al-Musnad” yake kupitia kwa Haywah bin Shurayh, kutoka kwa Baqiyyah.

[1] Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwa´iyf Sunan Abiy Daawuud” (3829).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (14/189)
  • Imechapishwa: 15/11/2020