Swali: Imethibiti kupitia kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ambaye amesema:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akibusu ilihali amefunga na akijichanganya ilihali amefunga.”

Je, hukumu ya busu hapa ni yenye kuenea kwa mzee na kijana au ni maalum kwa mzee peke yake?

Jibu: Hadiyth ni yenye kuthibiti kutoka kwa Mutme (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba alikuwa akibusu ilihali amefunga na akichanganyikana (يباشر) ilihali amefunga. Makusudio ya busu yanatambulika. Makusudio ya kuchanganyikana ni kuchanganyika kusikokuwa jimaa kama vile kupapasa. Kuhusu jimaa inaharibu swawm kwa andiko na maafikiano.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifanya hivo kwa sababu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa ni mwenye kuweza kujizuia nafsi yake na akitambua hukumu za swawm yake na akitambua (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yale yanayoiathiri na kuiharibu. Kuhusu watu wengine haitakikani kwao kufanya kitu kama hicho. Nakusudio kubusu na kuchanganyikana na mwanamke kwa kumbusu na kufanya mengineyo. Kwa sababu mambo hayo ni moja ya sababu inayopelekea kuharibu funga zao ukiongezea ujinga wao, unyonge wa imani zao na kutozidhibiti nafsi zao. Bora kwa muislamu ni yeye kujiepusha na yale yanayoamsha matamanio yake na yale anayochelea kuharibu swawm yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (02/404-405)
  • Imechapishwa: 16/03/2022