Ni jambo linalotambulika kwamba fikira za kuangamiza, misingi potofu na madhehebu  yaliyopinda ni mengi. Wanaoivika haki batili hawahesabiki. Vilevile walinganizi wa batili na waandishi wanaoandika katika kuzuia kutokamana na njia ya Allaah hakuna awezaye kuwahesabu isipokuwa Allaah. Wanawachanganya watu na batili yao kutokana na yale maneno wanayokengeusha. Wahubiri na wazungumzaji wamekuwa wengi katika redio na runinga. Katika kila uwanja katika vyombo vya habari kila mmoja anaita katika kundi lake, fikira yake, matamanio yake na anamkemea mwengine na kumwita katika batili. Hakuna njia ya kutoka katika mtihani huu isipokuwa kuupima juu ya mizani hii; Qur-aan na Sunnah. Tukiupima juu ya mizani hii mitukufu basi itachunguzwa na kutabainika haki kutokamana na batili, uongofu kutokamana na upotofu. Hivyo ndivo itashinda haki na watu wake na kutokomea batili na watu wake.

Walinganizi wa kikomunisti na wa kijamaa wanaopinga uwepo wa Allaah wakitanguliwa na wanaosema kuwa hakuna mungu na maisha ni pesa. Watu hawa wanakadhibisha haki na wanakanusha Kitabu cha Allaah na zile dalili za kiakili na za kinukuu zilizotajwa ndani yake kuhusu uwepo wa Muumba, uwezo Wake mkubwa na elimu Yake ilioenea. Rejea katika Kitabu cha Allaah na soma katika Aayah Zake yale yanayoelekeza juu ya alama ya uwepo Wake (Subhaanah) na kwamba Yeye ndiye mtengenezaji na mwenye kuhukumu vitu hivi (Subhaanah).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahamiyyat-ul-´Ilm https://binbaz.org.sa/discussions/33/اهمية-العلم-في-محاربة-الافكار-الهدامة
  • Imechapishwa: 16/03/2022